Najua ukianza kutaja list ya Tuzo ambazo mastaa wengi wamekuwa wakiingizwa kushiriki na kushindania, huenda jina la Tuzo za TFAA sio jina ambalo umelisikia mara kwa mara.
The Future Awards Africa (TFAA) ni Tuzo ambazo hutolewa kila mwaka kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-31 waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka husika, Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2004 na vijana wa Nigeria na mwaka 2015 zinatimiza miaka 10 ambapo kwenye list ya vijana waliotajwa kama Mabalozi waliowahi kushinda Tuzo hizo kwenye kipindi cha miaka 10, majina ya Watanzania wawili nayo yamo, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Patrick Ngowi.
Join patrick.ngowi at The Future Awards Africa 2015 as we celebrate 10 years of transforming lives.… https://t.co/FoH9OxU454
— The Future Project (@TFAAfrica) November 16, 2015
Join @diamondplatnumz Join The Future Awards Africa. Get involved in 10 more years of creating super… https://t.co/jmMk1A0JC8
— The Future Project (@TFAAfrica) November 16, 2015
List ya Mabalozi wote 10 waliowataja hii hapa
Bukola ‘Asa’ Elemide – Msanii wa muziki toka Nigeria
Michel ‘Don Jazzy’ Ajere – Producer wa muziki na msanii pia kutoka Nigeria
Tara Fela Durotoye – Mrembo kutoka Nigeria
Ndindi Nwuneli – Mwanzilishi wa Taasisi ya LEAP Africa iliyopo Nigeria
Nnaemeka Ikeguonu – Mjasiriamali wa masuala ya Kilimo Nigeria
Sangu Delle – Mwanaharakati kutoka Ghana
Patrick Ngowi – Mjasiriamali wa masuala ya nishati ya umeme wa jua kutoka Tanzania
Diamond Platinumz – msanii wa muziki kutoka Tanzania
Fogblanbenchi Lily Haritu – Mwanaharakati kutoka Cameroon
Oramait Alengoil – Mbunge kutoka Uganda
Kama unahitaji kuifahamu zaidi TFAA Awards unaweza kuingia hapa mtu wangu >>> TFAA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.