Shirikisho la soka Tanzania TFF February 23 limefanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuingia mkataba na Karibu Tanzania Association kwa ajili ya maendeleo ya soka la wanawake ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kuwa nyuma kwa upande wa Tanzania.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wameingia makubaliano na katibu wa TFF Selestine Mwesigwa na kusaini mkataba na Mia Mjengwa ambae ni mshauri wa Karibu Tanzania Association.
Mkataba huo ni endelevu na mafunzo ya soka yataanza kutolewa kwa shule za kijamii. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Rais wa TFF Jamal Malinzi aliomba watu kuwa watulivu na kusubiri hadi March 20 ndio kesi ya tuhuma za upangaji wa matokeo kwa michezo ya mwisho ya mechi za Ligi daraja la kwanza itasikilizwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE