Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi February 23 wakati wa kusaini mkataba wa kusaidia maendeleo ya soka la wanawake Tanzania na taasisi ya Karibu Tanzania, amezungumzia kuhusu tuhuma za upangaji matokeo katika michezo ya mwisho ya Ligi daraja la kwanza iliyomalizka hivi karibuni.
Jamal Malinzi aliyasema haya “Upangaji wa matokeo ni kosa kubwa katika soka, na halitakiwi kufumbiwa macho, TFF imeshitaki suala hili kwa kamati ya maadili ya TFF na majibu yatapatikana March 20, kuhusu mimi kuhusika huo ni uzushi, mimi naongoza taasisi kubwa siwezi kuunga mkono au kushiriki katika huo ujinga”
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE