April 5 2017 kulikuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinadai staa wa Hip Hop Bongo Roma mkatoliki kukamatwa na watu wasiojulikana jambo lililoibua hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa.
Leo April 6 2017 millardayo.com imemtafuta mmiliki wa Tongwe Records J. Murder ili kujua kama taarifa hizo ni kweli na kitu gani kinaendelea ambapo aliyasema haya…>>>“Ni kweli jana mida ya saa moja walikuja watu ambao hawajulikani wametokea wapi, wakaniulizia mimi pamoja na Roma japo mimi hawakunipata. Ikabidi wamuhoji Roma na wakaingia studio wakachua baadhi ya vitu na kuwachukua baadhi ya watu na kuondoka nao.
“Amechukuliwa Roma, Moni, Bello na kijana wa kazi wa mama yangu anaitwa Emma na hatujui wako wapi na wanahojiwa kitu gani, ila mpaka sasa napokea simu nyingi zikiwaulizia ndugu zao wako wapi, lakini mimi hadi sasa hivi sijui Roma yupo wapi.” – J. Murder.
Kusikiliza Bonyeza Play hapa chini…
VIDEO: Mr T Touch kuhusu Young Dee na dawa za kulevya….