Filamu ya vichekesho ya The Interview iliyotengeneza chini ya kampuni ya Sony imeweka rekodi ya kuwa ni filamu inayoendelea kupata mauzo mengi kutoka kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Sony Studio , The Interview imefanikiwa kuingiza dola milioni 31 baada ya mauzo kupitia mtandao na mifumo mingine ya mauzo ya filamu .
The Interview ambayo imezua utata wa kidiplomasia kati ya serikali za Marekani na Korea ya Kaskazini imeuzwa na kukodishwa kupitia mtandao zaidi ya mara milioni 4.3 kwa mujibu wa takwimu rasmi za Sony.
Takwimu hizi zimefanya filamu hii kuwa filamu iliyofanya vizuri kwenye mauzo kuliko filamu zote za Sony zilizoachiwa kupitia njia ya mtandao wa Internet ikiwa imeuzwa kuanzia December 24 mpaka January 4.
Takwimu hizi za mauzo hazijahusisha mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi za majumba ya sinema yapatayo 580 ambayo kwa upande wake yameingiza jumla ya dola milioni 5.
https://www.youtube.com/watch?v=dlPYvCv2bZ8
Filamu hii ilizinduliwa kwenye mtandao ambapo wateja wanaweza kuitazama kupitia Google Play, Youtube Movies, Microsoft Xbox Video, Itunes na mitandao mingine.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook