April 29 2016 Mbunge wa Muleba Kusini na aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amefanya Exclussive Interview na AYO TV na kuzungumzia hatua ya Rais John Pombe Magufuli kuanzisha Mahakama ya Mafisadi Nchini.
Profesa Tibaijuka anasema………>>>’Kwanza ukishaanzisha Mahakama unatafuta haki na ukweli, Watanzania wanahukumu kwa wepesiwepesi, sio kila mtuhumiwa ni mkosaji‘
>>>’Kwahiyo hili ni jambo zuri, sio kila mtuhumiwa ana kosa, kuna mitandao ya mafisadi inahakikisha kwamba haikamatwi na kuwapeleka wenzao mbele ndio inasema kafara, hivyo tunataka majipu yawe majipu haswa sio kukamua nyama tukamue majipu yenyewe‘
Yeye pia alikuwa na tuhuma za rushwa, anasemaje katika hili? …>>>’Ukweli ndio umeniweka hapa Bungeni, Wananchi wangu walielewa kuwa sio jambo nililohusika nalo, ikumbukwe mimi nilikuwa Waziri wa Ardhi na fedha zilitoka Benki kuu, sasa Waziri wa Ardhi na Benki kuu wapi na wapi?’
‘Ndio maana suala hili la kuwa na mahakama ni zuri sana, kwasababu kule Mahakamani ndio kuna nafasi ya kuujua ukweli‘
Unaweza kuipata full stori kwenye hii video hapa chini…
ILIKUPITA HII YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI BUNGENI KUHUSU MIZIGO KUPUNGUA BANDARINI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE