Leo April 24, 2018 Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ni Taasisi ya Umma na si Taasisi binafsi kama inavyosemwa.
Pia ameitaka TLS kutoingia kwenye uharakati wala siasa, kwani wakifanya hivyo watakosa ushirikiano na mahakama.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Prof. Juma amesema ameamua kuyasema hayo baada ya kuona mijadala kuhusu kauli yake aliyoitoa Ikulu April 20,2018 kwamba TLS ni taasisi ya umma.
Jaji Prof. Juma amesema TLS sio taasisi binafsi kwani hata ilipoanzishwa mwaka 1954 wakati bado kuna mkoloni Muingereza ambapo wanachama wengi walikuwa Wahindi na Wazungu walikuwa na maudhui ya maslahi binafsi.
Jaji Prof. Juma amesema baadaye maudhui hayo ya wahindi na wazungu, yaliondolewa baada ya uwepo wa mjadala kuhusu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 ambapo Wanasheria walianza kuzibadilisha baadhi ya sheria za chombo hicho.
“Hivyo nasisitiza kuwa TLS ni chama huru cha kitaaluma ambacho mawakili wanaotaka kufanya shughuli za Kiwakili lazima wapitie humo,” amesema Jaji Mkuu
Amesema taasisi hiyo imeanzishwa kisheria ili kufanya majukumu ya umma ambayo ni lazima iyafanye.
Jaji Prof. Juma amesema TLS imepewa majukumu mengi ya umma, ikiwemo kuboresha elimu na taaluma ya sheria Tanzania, ambapo majukumu hayo ni kazi ya umma na sio binafsi.
Pia amesema jukumu lao jingine ni kuisaidia serikali, bunge, mahakama na umma katika suala la kisheria.
“Hatuwezi kukubali kusema kwamba TLS wao ni chama binafsi,” amesema Jaji Mkuu Prof. Juma
Pia amesema hakupaswi kuwepo kwa malumbano kwani yakiwepo hawatafikia malengo.
“Hivyo ukiangalia majukumu ya TLS huwezi kuona siasa wala harakati bali ni masuala ya umma. TLS haipaswi kuingia kwenye uharakati wala siasa, na wakiingia huko hatutasa nhirikianao,” amesema Jaji Mkuu Prof. Juma
Rais Magufuli alivyokagua GWARIDE Dodoma