Kwa mara ya kwanza leo April 24, 2018 katika historia ya Uwanja wa Ndege Dar, Ndege kubwa ya ‘gorofa’ A380 ya Fly Emirates iliyokuwa ikielekea Mauritius ikiwa na abiria 475 wakitokea Dubai, imetua jijini DSM kwa dharura kutokana na hali mbaya ya hewa nchini humo.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna msaidizi, Matanga Mbushi amesema ndege hiyo ya Emirates, aina ya Airbus 380, EK701, ilishindwa kutua mara tatu nchini Mauritius kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha.
“Hiyo ndege ilikuwa ikielekea Mauritius, sasa hali ya hewa imekuwa mbaya ikashindwa kutua. Rubani alijaribu kutua mara tatu lakini akashindwa ndipo akaamua kuja Dar es Salaam kutua kwa dharura, kesho kama hali itakuwa nzuri wataondoka” amesema Mbushi
Rais Magufuli alivyokagua GWARIDE Dodoma