Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga kinachojulikana kwa jina la JOBO , Kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo hususani katika maeneo ya mwambao wa pwani ya kusini ,maeneo ya Lindi pamoja na maeneo ya Mtwara.
Kwa sasa kimbunga hicho kipo umbali wa takribani kilometa 930 kutoka pwani ya Lindi na takribani kilometa 1030 kutoka pwani ya Mtwara.
TMA imewataka wananchi kuchukua Tahadhari kwa kuzingatia Mwelekeo wa upepo na mawimbi makubwa ya bahari ambayo yanatarajiwa katika maeneo husika.