Mohamed Juma mkazi wa Barabara ya Kumi Jijini Tanga ambaye amekimbiwa na Mke wake wa ndoa kisa ni mtoto wao wa nne waliyemzaa akiwa na ulemavu hivyo imemlazimu yeye kumhudumia mtoto huyo kutokana na ulemavu wake alionao na kushindwa kutoka kwenda kujitafutia kipato jambo ambalo ni changamoto kwake kwani anakosa mahitaji ya mtoto na yake binafsi.