Tumesikia sana kuhusu waliotajwa kuwania tuzo za Grammy ambazo zitafanyika mwakani February 2015, lakini hii ninayokuwekea ni list ya albamu ambazo zimetajwa kufanya vizuri sokoni kwa mwaka 2014 japo sio mastaa wote wakali walioingia sokoni mwaka huu, kwani kwa jicho la haraka namuona msanii kama Rihanna amekaa benchi miezi yote 12 ya mwaka 2014.
Dada lao, Bey alifanya vizuri kwenye soko kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia album aliyoiita jina lake, wenyewe wanaiita ‘self titled album ‘, ikiwa na nyimbo kali kama ‘Drunk in Love’ aliyofanya na mumewe, Jay Z .
Ukiachilia mbali zile noma za kukaa jela, kuzinguana na mpenzi wake Karrueche , Mahudhurio ya Mahakamani na zile adhabu za Huduma za Kijamii ambavyo vimemuweka busy mwaka mzima, ‘X’ album ya Chris Brown iliyobebwa na ‘Loyal’ na ‘Fine China’. Mauzo yake wiki ya kwanza ilikuwa copy 146,000 huku kukiwa na fununu kwamba staa R. Kelly ni kama aliweka nguvu hivi kuproduce nyimbo kadhaa kwenye albam hii.
Sidhani kama lebo ya Rapa T.I, Hustle Gang wanajutia nguvu waliyoiweka kumsimamisha Iggy kutokana na mafanikio ambayo kayaonyesha mpaka sasa, tukianza na ule ushahidi wa Tuzo aliyoipata ya Favorite Rap/Hip Hop Album katika Tuzo za American Music Awards 2014.
Mafanikio sio mauzo pekee ya Album ama shows, kwa msanii Mali Music kuchaguliwa kushiriki tuzo kubwa kama Grammy kwenye Category ya Best Urban Contemporary Album ni mafanikio makubwa ambayo yataingia kwenye historia ya muziki wake ambao una ladha ya pekee, mchanganyiko wa Gospel, Soul na Hip Hop.
Msaada wa wakali kama producer Timberland na L.A Reid wakaweza kuzirudia baadhi ya nyimbo za Hayati MJ alizorekodi kuanzia mwaka 1983 mpaka 2001 kumefanya Dunia ipokee vizuri album yake ambayo imefanya mauzo ya copy zaidi ya mil.1 duniani kote mpaka sasa.
‘Because I’m Happy’ hakuna ambaye hakufurahishwa na kazi hii nzuri ya Pharrell kutoka kwenye albam yake ya GIRL , ameshakusanya tuzo nyingi lakini moja kati ya kubwa ni ile ya kupata kutambulika kuwa ‘Hollywood Walk of Fame’ na bado anawania tuzo nyingine 6 kwenye Tuzo za Grammy.
Mbali ya ugeni wake kwenye masikio na macho ya watu, haikuwa rahisi kupenya na kukubalika lakini tayari kapita na moja ya mafanikio ambayo yanazungumziwa ni yale ya Sam Smith kutajwa kuwania tuzo nyingine sita pia za Grammy, pamoja na wakongwe kama Pharrell na Beyonce.
‘Stronger’ ya Tank imeonyesha ile nguvu ambayo anayo baada ya kutoonekana kwenye climax ya muziki kwa kipindi kirefu akijihusisha na masuala mengine ikiwemo kucheza movie, album hii imetajwa kushika nafasi ya 13 kati ya album 200 bora za Billboard.
Join forces ya Toni Braxton na Babyface ambayo ilitengeneza nyimbo 11 kwenye album ya ‘Love, Marriage & Divorce’ haikuwaweka pabaya, album hii imekaa namba 4 kwenye Billboard top 200, huku mauzo yake yakiwa ni copy laki 4 mpaka sasa ndani ya Marekani pekee.
Mabibi na Mabwana.. Ile ‘Trigga ‘ ya Trey Songz ipo pia kwenye ile chache kali, imekaa namba moja kati ya 200 kwenye chati ya Billboard ikisaidiwa na hit song ‘Na Na’ huku mauzo yakiwa ni copy 260,000 mpaka sasa.
Kwako wewe ipi ni bora mtu wangu? Nitafurahi ukiniandikia comment yako.
Hakika nitakupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook