Maafa makubwa yametokea kwenye soka nchini DR Congo.
Angalau watu wapatao 15 ambao ni washabiki wa soka wamepoteza maisha kwenye mchezo wa TP Mazembe dhidi ya ASV Club.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Emmanuel Akweti, kwenye mahojiano na shirika la habari la Uingereza alisema kwamba:
“Mapolisi wanne walikuwa wakisumbuliwa na mashabiki. Walipoamua kupiga mabomu ya machozi, fujo zikaanza kuzuka na kusababisha vifo.”