Wakati Serikali ya awamu ya tano ikisisitiza kuwa na nchi ya viwanda, Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ‘TPSF’ Taasisi ya viwango Tanzania ‘TBS’ wameandaa tuzo za bidhaa bora za kitanzania ‘Top 50 Tanzanian Brands Awards 2016’ ili kufikia azma ya serikali ya kuwa na nchi ya viwanda.
Tuzo hizi zinatolewa ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wazalishaji wa ndani wa bidhaa kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia pato la Taifa, kutengeneza bidhaa bora, utoaji wa ajira, kukidhi mahitaji ya walaji urasi wa bidhaa zao na upatikanaji wake na pia ujaliji wa mazingira na jamii.
Lengo la mashindano hayo imeelezwa kuwa ni kubadili mitazamo ya walaji juu ya bidhaa za kitanzania dhidi ya sababu ya ubora hafifu na kuongeza uhitaji wa bidhaa za ndani.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
TPSF na TBS wamekuja na hizi tuzo ULIKOSA HAYA MENGINE YA KUFAHAMU KUHUSU USAFIRI WA NDEGE ZA EMIRATES? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI