Najua nina watu wangu ambao ni watembezi katika miji mbalimbali duniani na watataka kufahamu sheria za barabarani zinazotumika katika miji hiyo.
Sasa hapa nimekusogezea sheria 10 ambazo hutakiwi kuzivunja uendeshapo gari katika miji hii.
1: Chenzhen, China
Katika mji wa Chenzhen uliopo China dereva wa gari akikamatwa na kosa la kuwasha taa ‘full light’ bila sababu ya msingi adhabu yake ni kukaa mbele ya gari lililowashwa taa kwa dakika moja na kulipa fine ya Dollar 30. Adhabu hii imewekwa kama funzo kwa madereva ili kujua athari za kumuwashia mtu mwingine taa bila sababu.
2: Manila, Ufilipino
Katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila madereva wote wenye gari zenye plate number zinazoishia na namba mbili au moja hawaruhusiwi kuendesha gari siku za Jumatatu.
3: Arkansas, Marekani
Katika mji wa Arkansas uliopo Marekani ni kosa kisheria dereva kupiga honi akiwa maeneo yanayouzwa vinywaji baridi au katika vibanda vya kuuza sandwiches baada ya saa tatu usiku.
4: Colorado, Marekani
Ni marufuku kuendesha gari lenye rangi nyeusi siku za Jumapili ukiwa katika mji wa Colorado.
5: New Orlens, Marekani
Katika mji wa New Orlens, Marekani mwanamke harusiwi kuendesha gari mpaka mwanaume asimame mbele ya gari akiwa na bendera nyekundu ili kutoa angalizo kuwa kuna mwanamke anataka kuendesha gari hilo.
6: Ujerumani
Ni kosa la kisheria kuishiwa mafuta ukiwa unaendesha gari Ujerumani. Sheria hii imewekwa ili kuondoa magari ambayo yanasimamishwa barabarani kwa kisingizio cha kuishiwa mafuta.
7: Sweden
Nchini Sweden ni marafuku kuzima taa za gari hata ikiwa mchana. Madereva wa nchi hiyo wanatakiwa kuwasha taa za gari saa 24 hata ikiwa mwezi June ambapo jua huwa halizami katika maeneo mengi nchi humo.
8: California, Marekani
Ukiwa katika mji wa California ni kosa kwa wanawake kuendesha gari wakiwa wamevaa nguo za kulalia. Sheria hii ilikuja baada ya wanawake wengi kuvaa pajama hasa nyakati za asubuhi wakiwa wanapeleka watoto shule. Mtu atakayekiuka sheria hii anapigwa fine ya Dollar 22.
9: New Britain, Marekani
Ni kosa kuendesha gari kwa kasi 25 mhn hata ikiwa ni gari la zimamoto linawahi kuzima moto sehemu yoyote.
10: North Carolina, Marekani
Katika mji wa North Carolina, Marekani ni kosa kwa dereva kuendesha gari pembezoni mwa makaburi.
VIDEO: Ulimiss hii ya magari yaliyonunuliwa sana jijini Dar es Salaam? Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo