Mipango ya Rais Magufuli kuendelea kupambana na wabadhirifu wa mapato ya Serikali pamoja na zile jitihada za kuhakikisha Tanzania inakuwa na makusanyo mazuri ya mapato ya Serikali imekuja na good news leo January 06 2016.
Waziri mpya wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwahi kunukuliwa akisema ni aibu kwa kiongozi wa nchi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuomba misaada… jitihada za kukusanya mapato zimekuja na good news kwamba Mamlaka ya Mapato TRA yavuka lengo kwa kukusanya kodi Trilioni 1.4 mwezi Desemba 2015 baada ya jitihada za Rais Magufuli.
Kingine kilichonifikia leo kutoa kutoka kwa Kaimu Kamishna mkuu wa TRA Alphayo Kidata ni kuhusu malengo ya ukusanyaji kodi yaliyofikiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni baada ya kazi nzuri ya Rais kuwabana walipa kodi ambapo kwa sasa imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa mwezi Desemba ambayo ni zaidi ya trilioni1.4 kwa bara na visiwani.
“TRA imevuka lengo la makusanyo ya mwezi Desemba 2015 ambapo ilikusanya zaidi ya trilioni 1.4, mapato haya ni sawa na ongezeko la wastani wa bilioni 490 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba ambapo ni bilioni 900“- Alphayo Kidata, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA.
Kidata amesema kipindi cha Julai hadi Desemba 2015 TRA imekusanya zaidi ya trilioni 6 sawa na 95.5% ya makusanyo yote ambayo inatokana na mikakati mizuri ambayo wameiweka tangu Serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli iingie madarakani ikiwemo kuteketeza mianya ya upotevu wa mapato.
“TRA imekusanya zaidi ya bilioni 11 kutoka kwa wafanyabiashara hao, pia kuwa wafanyabiashara watano ambao bado hawajalipa kodi hiyo ya zaidi ya bilioni 2 na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao baada ya kuisha muda wa msamaha wa Rais“- Alphayo Kidata.
Kingine ni hiki kuhusu usajili wa pikipiki na bajaj kwa namba mpya >>>”Mpaka sasa jumla ya pikipiki na Bajaji 474,696 zimesajiliwa kati ya 610,461 kwa namba mpya, zoezi lilikumbwa na changamoto nyingi na tumeongeza muda wa mwezi mmoja kuhakikisha zote zinasajiliwa kabla ya jeshi la Polisi kuchukua hatua“- Kaimu Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE