Malalamiko ya siku nyingi ya wasanii wa kazi za tasnia ya muziki na filamu kuibiwa au kutumika isivyo kwa kazi zao na wao kutopata chochote kwenye kazi hizo yamesikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘ ambapo walianza kulifanyia kazi suala hilo kwa kufanya msako ili kubaini watu wanaoendesha biashara ya kuuza kanda za muziki na filamu bila kufuata utaratibu wa sheria.
April 19 2016 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘ imetoa taarifa kwamba zoezi la msako lilipelekea kukamatwa kwa jumla ya CDs na DVDs 656,579 zenye thamani inayokadiriwa kufikia bilioni 1.3. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa elimu kwa walipakodi , Richard Kayombo amesema ……….
>>>’katika zoezi hilo tulikamata wanaoshiriki kuuza kazi hizi kinyume cha taratibu, tulikamata mitambo 47 ya kudurufu CDs na DVDs pamoja na computer nne ambazo zinatumika katika ufanyaji wa kazi hiyo’:-Richard Kayombo
>>>‘Taarifa za kiinteligesia zinaonyesha kuwa bado kuna CD na DVD nyingi zimefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa hiyo zoezi hili ni endelevu na tutawafikia na kuwachukulia hatua za kisheria’:-Richard Kayombo
ULIIKOSA HOTUBA YA DIAMOND, ALI KIBA, NIKKI WA II, IDRIS NA JK MWENYEWE ALIVYOAGWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE