Familia za ndugu wa watu waliopata ajali kwenye ndege ya TransAsia Airlines GE235 ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege Taipei, wamekutana na uongozi wa Kampuni hiyo jana na kujadili mambo kadhaa ikiwemo malipo ya fidia na rambirambi za marehemu waliofariki katika ajali hiyo.
Liu Zhongji ni mwakilishi wa Kampuni hiyo ya ndege Taiwan, ametoa maelezo kuhusu kilichozungumzwa katika kikao kilichokaa zaidi ya saa tatu ambapo wanafamilia hao wamekataa kulipwa jumla ya dola milioni 14.9 za Taiwan (zaidi ya Ths. Milioni 850/-) ambayo wangepatiwa ndugu hao kwa kila mtu mmoja aliyefariki kwenye ajali hiyo.
Kiasi hicho cha pesa kilipangwa kutolewa kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi pamoja na rambirambi kwa wafiwa hao.
Ajali hiyo ilisababisha kifo cha watu 42, wengine 15 walifanikiwa kutoka salama huku mwili wa mtu mmoja ukiwa bado unatafutwa, ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya engine ya ndege hiyo kupata hitilafu na kuifanya ndege hiyo kupoteza mwelekeo, ikagonga ukingo wa daraja na kuanguka mtoni.
Janga lingine limewakuta marubani wa Kampuni hiyo ambapo baada ya ajali hiyo kutokea walilazimika kuwapa mtihani uliofanya 29 kati yao kusimamishwa kazi baada ya kufanya mtihani huo uliowapima namna wanavyoweza kupambana na kuokoa ndege iliyopata dharura.
Hii ni taarifa ambayo iliripotiwa kuhusu ajali hiyo FEBRUARY 4 na kituo cha CNN
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook