Huduma ya treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Bara ilisimama kwa muda kutokana na eneo korofi kati ya stesheni za kilosa Morogoro na Gulwe Dodoma lakini sasa hivi habari njema ni kwamba safari zinarejea kama kawaida sababu eneo hilo limetengenezwa.
Tarehe 1-5-2016 ndio safari zinaanza rasmi ambapo kusimamishwa kwa usafiri wa Treni kulisababisha abiria kupandia treni Dodoma badala ya Dar es salaam lakini sasa hivi treni ya kwanza ya Deluxe itaondoka kutokea Dar es salaam kwenda kigoma.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE