Raphael Warnock(51) wa Democratic amemshinda mgombea useneta wa Republican, Kelly Loeffler na kuandika historia yakuwa Seneta wa kwanza mweusi wa Georgia, Jimbo lililoundwa na urithi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Warnock amepata ushindi wa asilimia 50.6 dhidi ya asilimia 49.4 za mgombea wa Republican.
Warnock, hajawahi kushikilia wadhifa wa kisiasa aliochaguliwa hapo awali.
Tangu 2005, amekuwa mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Atlanta la Ebenezer Baptist, ambapo, Martin Luther King Jr alikulia kama mshiriki na baadaye mhubiri.
Warnock anajulikana kwa kufanya kampeni dhidi ya adhabu ya kifo na usawa wa uchum na kwa haki za uzazi za wanawake, haki za mageuzi ya polisi, na hatua juu ya shida ya hali ya hewa.
Hili linakuwa ni pigo jingine kwa chama cha rais anayeondoka madarakani, Donald Trump.