Rais wa Marekani Donald Trump ameteuliwa kuwania Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2021 na Mbunge mmoja wa siasa za mrengo wa kulia nchini Norway, akitaja jukumu la Trump katika kusimamia muafaka wa kurejesha mahusiano kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel.
Christian Tybring-Gjedde wa chama siasa za mrengo wa kulia cha Progress Party amesema makubaliano hayo yanaweza kuleta amani ya kudumu kati ya nchi kadhaa za Kiarabu na Israel.
Amesema anatumai kuwa Kamati ya Nobel yenye wanachama watano inaweza kuzingatia kile ambacho Trump amekifanya kimataifa na kuwa haitazuiwa na chuki zisizo sababu dhidi ya Rais huyo wa Marekani.
Mwanasiasa huyo wa Norway pia alimteua Trump mwaka wa 2019 akiutaja mkutano wa kilele wa Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un nchini Singapore 2018.
Via: DW Swahili.