Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia watu katika jimbo la North Carolina wapige kura mara mbili katika uchaguzi wa mwezi Novemba, licha ya kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Trump alisema wapiga kura watume kura kwa njia ya posta, halafu wapige kura binafsi ili kuujaribu mfumo wa upigaji kura.
Rais huyo mara kwa mara amekuwa akitoa madai kwamba kura zinazopigwa kwa njia ya posta zina uwezekano wa kuibiwa.
” Wacha watume kura na waache waende kupiga kura, kama mfumo ni mzuri kama wanavyosema basi bila shaka hawataweza kupiga kura yao binafsi .“ aliliambia Shirika la habari la North Carolina
Mkuu wa North Carolina Josh Stein ali-tweet kwamba “nimeshitushwa sana na kuwashashawishi ” watu katika jimbo “kuvunja sheria ili kumsaidia kupandikiza ghasia katika uchaguzi wetu “.