Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu ‘Twiga Stars’ Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo baada ya kuomba kwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF).
Kaijage aliiongoza Twiga Stars kwenye fainali za michezo ya Afrika (All Africa Games) zilizofanyika Congo Brazzaville Septemba 2015, baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.
TFF imesikitishwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye leseni daraja ‘A’ ya CAF, ambaye amekuwa akizinoa timu za taifa za wanawake ya ‘Twiga Stars‘ pamoja na timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite‘ tangu mwaka 2013.
Kinachofatia baada ya kocha Kaijage kujiuzulu, TFF inaendelea na programu za maendeleo ya soka kwa wanawake, ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake (Tanzania Women League).
TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.
Maandalizi ya mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Zimbabwe yataendelea chini ya kocha atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo utakaochezwa March 2016 na mshindi atacheza na kikosi cha timu ya Zambia.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo… https://t.co/P1mdpcTEQH
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) January 7, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.