Leo May 1, 2017 Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zimefanyika Kilimanjaro.
Katika kuadhimisha siku hiyo, TUCTA Mkoa wa Dar es Salaam imetoa ombi kwa serikali kuhusu wafanyakazi walioghushi vyeti wakisema kuwa kuna wajibu wa kuwatetea watu hao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa TUCTA Dar es Salaam, George Faustine amesema: “Sisi kama TUCTA hatutetei maovu, hatumtetei mvunja sheria yeyote nchi hii. Lakini tunathamini sana utu na heshima ya wafanyakazi. Kuna wajibu wa kuwatetea, lakini tunachoomba serikali iwatazame kwa jicho la huruma.”
Unaweza kubonyeza play kwenye hii video chini kutazama…
VIDEO: “Sio lazima mgeni rasmi awe Waziri” – Margaret Sitta ‘MB’. Bonyeza play kutazama…