Tukiwa bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015 najua nina watu wangu mnaotaka kufahamu kuhusiana na yale masanduku ya kupigia kura au mchakato wa kupigia kura, sasa hivi karibuni tumepata majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe.
‘Baada ya kupiga kura kituo cha kupigia kura kitabadilika na kuwa kituo cha kuhesabia Kura, kura zinahesabiwa kwenye kituo kilichopigiwa kura hakuna kuondoa yale masanduku pale kuyapeleka sehemu nyingine japo Sheria inaeleza kwamba ikitokea kwenye kile kituo kilichotumika kupigia kura kina giza haiwezekani kuhesabia pale‘ –Emmanuel Kawishe.
‘Mawakala wa vyama waliokuwepo pale na msimamizi wa kituo watashauriana, wakikubaliana wataenda kwenye kituo kilichokuwa karibu na zile kura zitatengwa pekee yake hazitachanganywa na zile nyingine… Kwa hiyo tunaamini kura zote zitahesabiwa katika kituo kinachohusika kupigiwa kura‘ – Emmanuel Kawishe.
‘Matokeo ya mgombea wa Urais yanatangazwa na tume ya Uchaguzi… Kura za Urais, Ubunge na Udiwani zitapelekwa kwenye kata ambapo zinaenda kujumlisha kura za kata zote kumtangaza mshindi wa Udiwani, zile za Ubunge na Urais zinapelekwa Jimboni zikifika pale jimboni Msimamizi wa Uchaguzi atazijumulisha’ –Emmanuel Kawishe.
‘Masanduku yale baada ya kuhesabu na kumaliza yanafungwa, na kwa wale mawakala waliokuwepo wanarekodi namba iliyoko pale, alafu masanduku yanapelekwa kwa msimamizi wa uchaguzi jimboni kwa ajili ya kuhifadhiwa’>> Emmanuel Kawishe.
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Emmanuel Kawishe akitoa ufafanuzi wote.