Taarifa iliyoripotiwa muda mfupi uliopita inahusu kuvamiwa kwa jengo la makumbusho lililopo karibu na bunge la Tunisia, huku kukiwa na ripoti kuwa watu 19 wamefariki katika tukio hilo, 17 kati yao walikuwa watalii.
Ripoti inasema kuwa wapiganaji walivamia bunge hilo wakiwa na nia ya kufanya shambulio.
Inasemekana kuwa kuna mateka ambao wameshikiliwa na wavamizi hao ndani ya jengo la kumbukumbu la Bardo ambalo liko jirani na Bunge hilo.
Shughuli za Bunge hilo ziliahirishwa baada ya hali kutokea kwa uvamizi huo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook