Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametumia maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika Mkoani Morogoro kuwataka Wanaushirika kuchukua hatua dhidi ya uharibifu wa mazingira nchini ili kuhakikisha kunakuwa na uendelevu wa shughuli za uchumi
Maadhimisho hayo ambayo ni ya 19 kuadhimishwa hapa nchini yalikuwa na kauli mbiu Ushirika kwa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, akifafanua kuhusu Kauli Mbiu hiyo Katibu Mkuu amesema ni wajibu wa Wanaushirika
kuhakikisha kuwa wanafuata kanuni na mbinu bora za utunzaji wa mazingira ili kuwa na uendelevu wa shughuli wanazofanya katika Vyama kwa kushiriki kwenye upandaji miti, kilimo mseto, kilimo cha umwagiliaji na jitihada nyingine nyingi
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiongea na wanaushirika katika maadhimisho hayo ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika kuhakikisha kuwa wanafanyakazi kuhakikisha kuwa wanaushirika wananufaika na shughuli zinazofanywa na Vyama hivyo hususani mali za Ushirika ili mwanachama mmoja mmoja apate manufaa na chama.