Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Desemba 20, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Magereza ya Keko, Ukonga na Segerea yalemewa wafungwa na mahabusu, Serikali yaamua kuunda kamati kushughulikia taasisi hiyo #MWANANCHI DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Polisi K’njaro imemtia mbaroni mtuhumiwa wa makosa ya kimtandao ambaye anadaiwa kutumia jina la Balozi SEFUE kutapeli viongozi #MWANANCHI

Kikao cha Baraza la madiwani wa jiji la Tanga cha kumchagua meya na naibu wake jana kiliishia kwa wajumbe kupigana ngumi #MWANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Aliyekuwa mgombea Urais UKAWA, LOWASSA amesema anashangaa anaambiwa ameleta vurugu wakati dunia inamkubali ni mlinzi wa amani #MWANANCHI DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri wa Katiba MWAKYEMBE amesema Rais amempa kazi ya kuhakikisha anakamilisha mchakato wa katiba pamoja na mahakama ya rushwa #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri wa Nishati na Madini MUHONGO amewataka wawekezaji wa ndani wenye uwezo wa kuwekeza kwenye umeme kujitokeza kuwania zabuni #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri Mkuu MAJALIWA ametaka miundombinu ya mabasi yaendayo kasi iboreshwe na kupendekeza viyoyozi viwekwe vituoni #MWANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Polisi imefafanua taarifa za kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya askari wametajwa kuwa wana vyeti bandia #MWANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Wasafiri wa kituo cha Mabasi Ubungo wamelalamikia adha ya usafiri ktk kipindi hiki cha sikukuu,walazimika kupanda Noah na Coaster #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumchinja mkuu wa Idara ya ulinzi na usalama TANAPA,mwili wake wakauweka kwenye buti la gari yake #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Baadhi ya wakazi waliovunjiwa nyumba zao ktk bonde la mto Msimbazi wameshindwa kuhama eneo hilo na kuweka mahema ili kujihifadhi #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Hospitali ya rufaa KCMC inahitaji mablanketi 2,000 ili kuweza kuhudumia wagonjwa wote wanaolazwa #MWANANCHI #DEC20 https://t.co/007p6jEkrX
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Mwanasiasa mkongwe Juma DUNI amesema hatima yake ya kubaki au kuondoka ndani ya CHADEMA itajulikana mwezi ujao #MWANANCHI#DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Mbunge wa Nyamagana amemwomba Waziri wa afya kuishawishi Serikali kuitengea bajeti hosp. ya Bugando kwa 100% ili kuboresha huduma #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Mjumbe wa CCM Butiama amelaani tamko la Tundu LISSU kuwa Prof. MUHONGO hakutakiwa kupewa Uwaziri kutokana na kashfa ya Escrow #MWANANCHI DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa sugu Kigoma baada ya jitihada za kuukabili kugonga mwamba #MWANANCHI DEC20 https://t.co/007p6jEkrX
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Wadau wa elimu wamewatuhumu baadhi ya walimu ni chanzo cha mimba za utotoni kwa kuwarubuni wanafunzi na kuficha takwimu zao #MWANANCHI DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
RC Simiyu amewataka Madiwani kuacha tabia ya kujikweza na kujiita waheshimiwa kwa kuwa inajenga tofauti kati yao na wapigakura #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
TFDA kanda ya Ziwa imekifungia kiwanda cha kusindika samaki kutokana na kushindwa kusajiliwa na mamlaka hiyo #MWANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Takataka zilizokusanywa na wananchi wa Karagwe siku ya Uhuru hazijatolewa na mkandarasi wa Mamlaka ya mji huo mpaka sasa #MWANANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Mtoto wa miaka miwili aishi na maiti ya mama yake kwa siku 2 Marekani, mama yake alifariki gafla akiwa ndani ya nyumba yake hiyo #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Wanyarwanda wameunga mkono kwa wingi marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu Rais wao Paul KAGAME kuendelea kuongoza #MWANANCHI #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri wa Nishati Prof.MUHONGO amesema kuanzia mwezi ujao bei ya umeme itashuka kutokana na kushuka bei ya mafuta ktk soko la dunia #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri Mkuu MAJALIWA ameitaka ofisi yake kupitia upya mikataba ya kampuni zote zilizoingia zabuni ya kuendesha mradi wa BRT #TzDAIMA #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Wananchi wa Masasi na Ludewa wanatarajia kumchagua Mbunge leo atakayewawakilisha Bungeni baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo #TzDAIMA #DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
LOWASSA amesema hataki kwenda Ikulu huku mikono yake ikibubujika damu na kamwe hataweka mbele masilahi binafsi kusaka madaraka #TzDAIMA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
TFF inatarajia kumfikisha kwenye kamati ya maadili Jerry Muro kwa kauli za kibaguzi dhidi ya Ofisa habari wa Simba Haji Manara #TzDAIMA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri Mkuu MJALIWA amewataka watendaji wa mradi wa DART na wadau wote kuhakikisha mradi huo unaanza kufanya kazi January10 #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Watu wasiojulikana wamesambaza taarifa za uongo zinazolichafua jeshi la Polisi ktk mitandao ya kijamii wakidai zimetolewa na jeshi#MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Serikali imezindua kamusi kuu ya Kiswahili Tanzania iliyochukua miaka 12 kuandaliwa, imezingatia matumizi mapana ya lugha #MTANZANIA #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Kasi ya Rais MAGUFULI imewageukia wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa ikiwa ni utekelezaji wa alivyoahidi kwenye kampeni #NIPASHE #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri mkuu mstaafu Cleopa MSUYA jana alikuwa Waziri wa tatu akiongozwa na LOWASSA, SUMAYE kukosoa mwenendo mbaya wa CCM #NIPASHE #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema hana mpango wa kuihama klabu hiyo lakini ikitokea akapata timu nyingine atakwenda #GazetiDIMBA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Baadhi ya makocha wa ligi kuu Tz wameunga na wenzao duniani kutoa hisia zao juu ya kutimuliwa kwa kocha wa Chelsea MOURINHO #GazetiDIMBA
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Askari wa jeshi la Polisi wakiwa na silaha wamevamia kanisa moja Dar huku ibada ikiendelea na kisha kumchukua mchungaji #GazetiNYAKATI DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Malori zaidi ya 50 ya magunia ya mahindi kutoka Kenya yaliyoingia nchini kupitia Sirari yakwama kwa zaidi ya saa nne #MZALENDO #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
RC Kagera amewataka kina mama wenye umri wa kuzaa watumie njia za uzazi wa mpango ili kuwafanya watoto wawe na afya nzuri #MZALENDO #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Serikali imeondoa urasimu katika sekta ya Nishati na kukaribisha wawekezaji katika miundombinu ya uzalishaji umeme #MZALENDO #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Jeshi la Polisi Katavi limewataka wananchi kuimarisha usalama wa maisha na mali zao, washirikiane kutoa taarifa za uhalifu #HabariLEO #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Halmashauri ya Wilaya ya Longido imefanikisha kuvunja ndoa bubu za wananfunzi wawili walioachishwa masomo na wazazi wao #HabariLEO #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Waziri Kairuki ameitaka idara ya uchambuzi wa kazi kuwianisha mishahara ya watumishi ili kusiwe na tofauti kati ya wa juu na chini #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Kocha Mourinho aandaliwa ulaji klabu ya Man United baada ya kutimuliwa Chelsea, mmiliki wa Chelsea asema hakupanga kumtimua #NIPASHE #DEC20
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Mamalishe zaidi ya 500 katika soko la Majengo, Dodoma wamemtaka Rais MAGUFULI kufuta agizo la TAMISEMI la kubomoa vibanda vyao #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) December 20, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.