Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la JamboLeo yenye kichwa cha habari ‘Mfungwa adaiwa kuuawa kwa kipigo’
#JamboLEO Mfungwa John Okol, anadaiwa kuuawa kwa kipigo cha mkuu wa gereza la keko Kamishna msaidizi Abdallah Kiange pic.twitter.com/j1Dk4XNFN5
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuwa mfungwa namba 79 ya mwaka 2016 John Okol, anadaiwa kuuawa kwa kipigo cha Mkuu wa Gereza la Keko, Kamishna Msaidizi Abdallah Kiange.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa ndugu wa marehemu zilidai kuwa kifo cha ndugu yao kilichangiwa na kipigo cha Mkuu huyo kwa kilichodaiwa Okol na wenzake wanatumia simu gerezani, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, ndugu hao walidai kuwa tuhuma kwamba wafungwa hao wanatumia simu gerezani zinapaswa kuelekezwa kwa askari Magereza wanaowalinda na kuwa watumishi hao ndio huuzia simu wafungwa.
Kupitia gazeti hilo ndugu walisema zipo taaarifa kuwa wanaohusika na uingizaji wa simu gerezani na kuwauzia wafungwa ni askari wa kikosi cha ukaguzi. Taarifa kutoka ndani ya gereza hilo zilieleza kwamba baada ya tukio la kupigwa na kuwa na hali mbaya, baadhi ya wafungwa waliomtaarifu ofisa usalama wa gereza hilo, Koplo Rashid kuhusu hali yake lakini inadaiwa akasema alikua anadanganya kuugua lakini usiku wa kuamkia jumanne alipoteza maisha.
Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, licha ya kukiri kutokea kwa kifo hicho, Kamishna Kiangae alikanusha kusababishwa na kipigo akisema mfungwa huyo alikua akiugua athma na malaria na habari za kupigwa hazina ukweli wowote.
Kamishna Kiange alisema mfungwa huyo amekua akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu na kabla ya kifo alizidiwa ghafla…..>>>”Ni kweli kuna mfungwa amepoteza maisha lakini kifo chake hakihusiani na kupigwa alikua anaumwa athma na malaria na kwa muda mrefu amekua akiishi bila kufanya kazi kubwa”
Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania leo July 06 2016
#JamboLEO TRA yasisitiza benki, taasisi za fedha kutotoza wananchi VAT kwa miamala wanayofanya pic.twitter.com/VX2BjN146b
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#MWANANCHI Ajifungua watoto watatu Muhimbili, azuiwa wodini hadi atakapolipa deni la sh. 540,000 pic.twitter.com/TLXhtC5myr
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#MWANANCHI Utafiti Twaweza wabaini 53% Tanzania bara hawajui kilichojiri Z'bar tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu 2015 pic.twitter.com/mIrT0kR1Be
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#TanzaniaDAIMA Imeelezwa kuwa wanawake wanaongoza kwa matumizi ya shisha huku Dar ikiwa kinara ikifuatiwa na Arusha pic.twitter.com/4qxFtfoPo3
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#TanzaniaDAIMA TRA yavuka lengo la makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, yakusanya trilioni 13.3 pic.twitter.com/TSRz6jrUx0
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#TanzaniaDAIMA Bei za mafuta zapanda ambapo petrol itauzwa 1888, dizeli 1720 na mafuta ya taa 1687 kwa rejareja pic.twitter.com/PhVGnR1uE2
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#TanzaniaDAIMA SUMATRA imeyafungia mabasi 12 ya kampuni ya City Boys ili kupisha uchunguzi pic.twitter.com/X9MMlylCzK
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#NIPASHE Matapeli sasa wanakodisha magari na baadaye kuyauza bila idhini ya mmiliki na kutorokea kusikojulikana pic.twitter.com/HaFqo6N8Eq
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#MTANZANIA Wafanyabiashara wawili wamehukumiwa jela miaka mitatu au faini mil 1.5 kila mmoja kwa kutokuwa na EFDs pic.twitter.com/WNeXFeEOjN
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#NIPASHE TRA kukagua wafanyabiashara mtaa kwa mtaa kama wanatumia mashine za kielektroniki za kodi 'EFD' pic.twitter.com/2OaEDrewZt
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
#JamboLEO Wabunge UKAWA kwenda mahakamani baada ya kunyimwa posho kutokana na kuingia bungeni kusaini kisha kutoka pic.twitter.com/0IoutJi6F0
— millardayo (@millardayo) July 6, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 06 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
https://www.youtube.com/watch?v=fQ1Okmw8ivw