Mitandao ya Kijamii ni kiungo kikubwa sana siku hizi kwa watu kutoka maeneo mbalimbali Duniani, jamaa wanaomiliki Mtandao huu nao huwa wanakaa na kufanya tathmini zao kuangalia jinsi ambavyo Mtandao wao unakubalika.
Twitter ilizinduliwa rasmi kabisa March 2006 ndani ya San Francisco Marekani, mpaka sasahivi tunahesabu kama miaka 9 hivi iliyopita… kwenye Ripoti yao ya June 30 2015 walipata Takwimu ambazo nimeona nikusogezee hapa kama hukuwahi kuzijua, basi taarifa hii ikufikie.
1. Hesabu ya Watumiaji wa Twitter kwa Mwezi>>>Ripoti yao inaonesha kuna watumiaji 316 wa Mtandao wa Twitter ambao wako active kabisa kwa kila mwezi Dunia nzima.
2. Idadi ya Tweets Kila Siku >>> Unaambiwa kuna wastani wa #Tweets Milioni 500 kwa kila siku Duniani, kama na wewe ni mtu wa kutweet basi ujue na yako pia jamaa wameihesabu !!
3. Watumiaji wa Twitter Kwenye Simu Zao >>> Kutoka kwenye idadi yote ya watumiaji wa Twitter, asilimia 80 kati yao wanatumia simu za mkononi huku wengine wakitumia vifaa vingine kama iPad na Computer.
4. Idadi ya Wafanyakazi Wao >>> Ripoti yao inaonesha wana jumla ya wafanyakazi 4,100 kwenye maeneo mbalimbali Duniani.
5. Idadi ya Ofisi Zao >>> Twitter wamethibitisha kwamba wana Ofisi zao kwenye maeneo zaidi ya 35 Duniani, kwa hiyo sio kwamba kila kitu kinafanyika na kusimamiwa Marekani… Baadhi ya maeneo ambako Twitter wana Ofisi zao ni kama Dubai, Dublin, Hamburg, Hong Kong, Jakarta, London na Madrid.
6. Watumiaji wa Twitter Nje ya Marekani >>> Takwimu zao zinaonesha kuna watumiaji 77% wa Mtandao huo ambao wako nje ya Marekani.
7. Lugha Unazoweza Kutumia Twitter >>> Uthibitisho mwingine ambao wamiliki wa Twitter wameutoa ni kwamba kuna lugha zaidi ya 35 ambazo watumiaji wa Mtandao huo wana uhuru wa kutumia, kuanzia kwenye maelekezo mpaka tafsiri ikitokea kuna maneno huyaelewi.
8. Taaluma ya Wafanyakazi >>> Kwa sababu Mtandao wenyewe unaendeshwa na masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano, 50% ya Wafanyakazi wa Twitter ni Engineers !! Hiyo ni kawaida, yani ni sawa na Hospitali ambako asilimia kubwa ya Wafanyakazi ni wataalam wa masuala ya kitabibu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE