Kocha wa Man City Pep Guardiola ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwa bora kwa sasa hususani, uwezo wake wa kushinda mataji akiwa na vilabu mbalimbali Ulaya, Pep Guardiola ambaye amewahi kufundisha pia vilabu vya FC Barcelona na FC Bayern Munich anatajwa kama mmoja kati ya watu wanaosababisha bei za mafuta ya magari kupanda (Petrol/Diesel).
Rais wa club ya FC Bayern Munich, Uli Hoeness ameeleza kuwa Pep Guardiola akiwa anahitaji kumsajili mchezaji mwenye thamani ya euro milioni 100 na zaidi huwa anachukua clip video za mchezaji husika na kumpelekea Sheikh Mansour ambaye ndio mmiliki wa Man City na mmiliki wa biashara ya visima vya mafuta uarabuni.
“Rafiki ya Pep aliniambia huwa kinatokea nini kama anakuwa anamuhitaji mchezaji mwenye thamani ya euro milioni 100 na kuendelea, anakusanya baadhi ya video za mchezaji huyo na anaenda kuonana na sheikh, siku inayofuatia Sheikh anaongeza bei ya mafuta kidogo ili apate pesa za usaji wa mchezaji husika”>>> Rais wa FC Bayern Munich, Uli Hoeness
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!