Staa wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Tyga ni miongoni ya wasanii wanaofunga mwaka wa 2015 na excluvise interviews na mitandao pamoja na majarida mbalimbali ya burudani… Nimekutana na interview ya rapper huyo na mtandao wa Yahoo na ndani yake amegusia vitu vingi ikiwemo maana ya jina la ‘Tyga’ , umaarufu na mengine kibao.
Haya ndiyo niliyofanikiwa kuyanasa kupitia interview ya Tyga na mtandao wa Yahoo:
Maana ya jina lake la kisanii Tyga: “Tyga inamaanisha ‘Thank You God Always – T.Y.G.A’ na ni jina lilotokana na tabia ya mama yangu kupenda kuniita Tiger Woods nikiwa mtoto kwa sababu kwa kipindi hicho naambiwa nilikuwa nafanana sana na mchezaji huyo mwenye umaarufu mkubwa duniani..“
Anachukuliaje umaarufu: “Umaarufu ni baraka na kwa wakati huohuo umaarufu unaweza kukuletea tabu maishani… Ukiwa maarufu kuzoea hali ya kila mtu na camera na waandishi wa habari kukufuata kila sehemu ni ngumu, uwe rapper, msanii wa R&B, mwigizaji au hata mwanamichezo maarufu huwezi kuzoea… lakini ndio maisha tuliyochagua, tumechagua kujitoa na kujiweka hadharani na kujinyima uhuru wetu binafsi…“
Ulitambua lini kuwa unataka kuwa msanii wa HipHop: “Nadhani nilikuwa na miaka 12… nilikuwa narekodi nyimbo zangu chumbani kwangu kwa kutumia beats nilizotengeneza kwenye laptop yangu na nilikuwa nafanya tu freestyles lakini sikuwahi kumsikilizisha mtu yoyote. Ilikuwa kila siku nkitoka shule nawahi nyumbani kujirekodi hata kucheza na marafiki zangu nilikuwa sitaki.. nilikuwa nataka kutengeneza muziki tu!“
Tofauti ya muziki wake na muziki wa wasanii wengine wa HipHop: “Licha ya kwamba watu wengi wanafanya muziki, nahisi kile nachofanya mimi hakiwezi kulinganishwa na kile anachofanya rapper mwengine, kwa sababu naanmini ukianza kujilinganisha na mtu au watu unakuwa unapoteza imani na kile unachokifanya au unachotakiwa kukifanya.”
Hizi ni baadhi ya picha alizozipiga Tyga kwenye photoshoot yake na mtandao wa Yahoo:
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.