Leo February 25,2019 Muigizaji bora wa kike Flora Kiyombo na Muigizaji bora wa Kiume Rashidi Kassim walioshinda tuzo za SZIFF siku ya Jumamosi wamefanyiwa mahojiano na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena na kuwataja Wema Sepetu na Hemedy kama tishio.
“Mimi nilikiwa namuhofia @wemasepetu sababu yeye ni msanii wa muda mrefu na amefanya filamu nyingi na kingine anamashabiki wengi hivyo kwake ingekuwa rahisi kushinda sababu ya umaarufu wake lakini nashukuru Mungu kwa kuweza kushinda Msanii bora wa kike”Flora. Huku Rashidi yeye ndiyo mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kiume amesema ” Mimi nilikuwa namuhofia @hemedyphd kwa sababu ni msanii anayejulikana na yupo kwenye filamu muda mrefu”
“Sijasikia, sijui kama watu wananiita Kamwene, Kamwene ni salamu hivyo sioni haja ya watu kuniita hivyo, kwenye filamu ya #Kesho kipande ambacho kilikuwa kigumu kwangu kuigiza ni wakati nalia makaburini, maana kulia bila kupigwa ni kazi hivyo ilibidi nivute hisia ya msiba wa marehemu baba yangu mkubwa” Flora Muigizaji bora wa kike
EXCLUSIVE: Watoto waliowapiga chini Wema, Monalisa, Gabo kipengele cha Muigizaji Bora