Club ya Man United ya England imethibitisha kuwa beki wao wa kimataifa wa Ivory Coast Eric Bailly ataendelea kukaa nje ya uwanja, akiendelea kuuguza majeraha ya goti lake la kulia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea Jumapili iliyoisha na kujikuta wakitoka sare ya kufungana 1-1.
Bailly aliumia goti lake la kulia baada ya kugongana na Mateo Kovacic katika mchezo huo na kushindwa kumaliza game na kutolewa nje dakika ya 51 na nafasi yake ikachukuliwa na Marcos Rojo, baada ya mchezo huo kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alianza kuonesha hofu kuwa watamkosa mchezaji huyo hadi mwisho wa msimu.
Sasa ni wazi kutokana na jeraha hilo Bailly atakuwa nje uwanja hadi mwisho wa msimu lakini atazikosa fainali za mataifa ya Afrika 2019 zitakazofanyika nchini Misri, timu ya Ivory Coast inayochezewa na Eric Bailly imepangwa Kundi D lililo na timu za Morocco, South Africa na Namibia.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23