Idara ya uhamiaji ya nchini Libya May 30, 2018 iliwaandalia zaidi ya wahamiaji haramu 1,300 futari kwenye kituo kimoja cha kupokea wahamiaji mjini Tripoli.
Karamu hiyo ilihudhuriwa na mkuu wa idara hiyo Mohamed Beshr pamoja na mabalozi wa nchi zingine walioko nchini humo.
“Karamu hii ya futari inalengwa kuonyesha upendo na undugu kwa wahamiaji haramu. Hafla hii pia inawapa wahamiaji fursa ya kuwa karibu na mabalozi wa nchi zao,Wahamiaji wote, waislamu au wasiokuwa waislamu wamealikwa kufuturu nasi,” alisema Beshr