Hatimae muda wa furaha umeisha ndani ya club ya Real Madrid ikiwa ni siku moja imepita toka kiungo wa timu hiyo Luka Modric kukiri kuwa timu yao haina mbadala wa Cristiano Ronaldo na wanamkumbuka sana, pia Real Madrid imempoteza kocha wao aliyewaweka katika rekodi ya kihistori na kuwapa Ubingwa wa UEFA Champions League mara tatu.
Real Madrid ikiwa inacheza msimu wake wa kwanza wa UEFA Champions League bila uwepo wa Cristiano Ronaldo wamejikuta wakitolewa katika michuano hiyo na kuvuliwa Ubingwa huo baada ya kutwaa mara tatu mfululizo, kufuatia kipigo cha magoli 4-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu, ushindi wa ugenini wa 2-1 waliowafunga Ajax wiki mbili zilizopita haujawa na msaada kwao.
Hivyo Real Madrid wamejikuta wanaondolewa katika michuano hiyo kwa ushindi wa Ajax wa jumla ya magoli 5-3, Real Madrid baada ya kutolewa leo katika hatua ya 16 bora ndio wanakuwa wametolewa kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo katika hatua ya mapema zaidi, kwani kwa miaka 9 toka (2010-2011) hawajawahi kutolewa hatua ya 16 bora au robo fainali.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake