Leo December 8, 2018 Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefika na kufyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajaji mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa operation ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji.
“Sasahivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapingua” -Ngonyani.
“Tumeamua kusimamia sheria hatutawabakisha, leo tunafyeka mazao yote yaliyopo ndani ya Mita 60 lakini kinachofuatia nyumba ambazo zipo ndani ya Mita 60 zenyewe pia tutazifanyia kazi”- Ngonyani.
KUTANA NA MTANZANIA ASIA MUSTAFA ANAEISHI BILA YA FIGO ZOTE MBILI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA