Mahakama ya Rufaa Tanzania imeyafuta maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutaka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kufuta shtaka la ugaidi lililokuwa linamkabili Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.
Maombi hayo yamefutwa na Jaji Mussa Kipenka baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka kueleza kwamba DPP ameamua kuondoa kibali cha maombi hayo kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Kutokana na hatua hiyo Lwakatare ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA anakabiliwa na kosa moja la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky kwa kutumia sumu ambalo kesi hiyo ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mtazame kwa kuplay video hii Mbunge Lwakatare baada ya maamuzi ya Mahakama ya Rufaa!!!
https://youtu.be/mbeGld7t-7Y
ULIPITWA na huu UFAFANUZI wa Utapeli ulivyoibuka ‘Law school of Tanzania’ na mmoja kukamatwa? Play kwenye video hii!!