Mwigizaji wa tamthilia ya Empire Jussie Smollet ameachiwa kwa dhamana kufuatia kushikiliwa na Polisi kwa masaa kadhaa na kisha kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kuwadanganya Polisi.
Polisi wamezungumza na kusema kuwa mwigizaji huyo alipanga kitendo hicho cha kushambuliwa mjini Chicago kutokana na kutoridhishwa na malipo anayolipwa kwenye tamthiliya ya Empire na hivyo kuchukua maamuzi ya kuwadanganya Polisi kuwa amefanyiwa vitendo vya kibaguzi.
Inaelezwa kuwa Jussie Smollet alituma barua ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa mapenzi ya jinsia moja kwa kampuni ya Fox studio anayofanya nayo kazi siku moja kabla ya shambulio huku ikiripotiwa kuwa Jussie Smollet alijisalimisha mikononi mwa polisi siku ya Alhamisi ili kusikiliza mashtaka yake ya kuwadanganya polisi kuhusu kutekwa.
Hata hivyo Jussie Smollet amekana mashtaka yote na kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 233 za Kitanzania .
“Watu wanachotakiwa kuskia ni ukweli, nilihisi kuna kamba shingoni mwangu na nikaanza kupiga kelele, waliniita mtu mweusi na hakuna sehemu ambayo ungeweza kuikata hiyo kamba, kama ningesema mimi ni muislam, Mmexico au mtu mweusi nahisi watu wengi wangenipa ushirikiano”
MAPYA KESI YA WEMA: VIDEO YAKE YA NGONO YACHAMBULIWA MAHAKAMANI