Club ya Sevilla inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Tanzania May 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki iliyoandaliwa na kampuni ya michezo SportPesa kwa ushirikiano na LaLiga, Sevilla FC itacheza na mabingwa wa Tanzania Simba SC, hiyo itakuwa ni changamoto kwa Simba SC kujipima uwezo kwa kucheza na timu iliyowahi kushinda taji la Europa League zaidi ya mara mbili.
Mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa siku ya Alhamisi May 23 kuanzia saa moja kamili usiku kwa viingilio kuanzia 5000 na zinapatikana kwenye vituo vyote vya mafuta PUMA pamoja na Selcom, Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas alisema
“Kupitia ujio wao timu ya Sevilla watafanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kuinua sekta ya michezo nchini kwa vijana na mpira wa miguu kiujumla, Watatoa mafunzo ambayo yatahudhuriwa na timu ya vijana ya Bom Bom FC katika uwanja wa Uhuru bila kusahau semina elekezi itakayotolewa na maofisa wa club ya Sevilla kwa viongozi wa vilabu, TFF na washirika wake ili wapate kuimarika kitaaluma na kupata uelewa jinsi ya kuongeza mapato ya club zao”>>>Tarimba
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF Bwana Salum Madadi amesema Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Herry Sasii ameteuliwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuchezesha mechi kati ya Simba na Sevilla FC,Sasii atasaidiwa na Mohammed Mkono kutoka mkoa wa Tanga na Soud Lila wa Dar es Salaam, mwamuzi wa akiba atakuwa Jonesia Rukyaa kutoka mkoa wa Kagera.
“Waamuzi wanaochezesha mchezo huu wote ni Waamuzi wenye beji za FIFA, mchezo huu mbali ya kujitangaza kama nchi lakini pia ni sehemu ya kutangaza vitu vyetu mbalimbali wakiwemo wachezaji na Waamuzi”>>>Madadi
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC