Ubalozi wa Marekani nchini Urusi umewataka Raia wa Marekani waliopo nchini humo kufikiria kuondoka mara moja kutokana na idadi ndogo ya safari za ndege zinazowasili na kuondoka ndani ya Taifa hilo.
“Idadi inaongezeka ya Mashirika ya ndege yanayoghairi safari za ndani na nje ya Urusi na nchi nyingi zimefunga anga zao kwa Mashirika ya ndege ya Urusi hivyo Raia wa Marekani wanapaswa kufikiria kuondoka Urusi mara moja kupitia nafasi ambazo bado zinapatikana”
WANANCHI WA UKRAINE WAKABIDHIWA SILAHA, WAINGIA NAZO MITAANI KUWAKABILI URUSI
KOREA KASKAZINI WARUSHA KOMBORA JINGINE, VIPI KUHUSU URUSI NA UKRAINE?