Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Magonjwa Sita yatikisa nchi’
#JamboLEO Magonjwa yanayosumbua Taifa yametajwa kuwa ni malaria, UKIMWI, kifua kikuu, kisukari, moyo na selimundu pic.twitter.com/Q6omMJtyZS
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
Gazeti la Jambo Leo limeripoti kuwa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto imetaja magonjwa makuu sita; kuwa ndiyo yanayolisumbua taifa kwa sasa. Magonjwa hayo ni matatu ya kuambukiza, ambayo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla ni malaria, UKIMWI, kifua kikuu, kisukari, moyo na selimundu.
Kigwangalla aliyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hilo na kusema magonjwa hayo ni hatari yanapaswa kuchukuliwa hatuaza haraka na dharura kuyadhibiti kwani ndiyo yanayoongoza kwa vifo vya watu wengi zaidi ikilinganishwa na mengine.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania
#MWANANCHI Ikulu kuhakiki upya vyeti vya wakurugenzi wa halmashauri baada ya awali kutumia nakala za vyeti vyao pic.twitter.com/8BOXBc3f1u
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#MWANANCHI Mashirika haki za wanawake yasema uteuzi nafasi za uongozi serikalini hauzingatii uwakilishi wa kijinsia pic.twitter.com/sLjIifduje
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#MWANANCHI Mhasibu mkuu jeshi la polisi asimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya posho ya chakula kwa wasio askari pic.twitter.com/uZL4kbIF5x
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#MWANANCHI Wanunuzi pamba wagoma ili kuishinikiza Serikali kuondoa ongezeko la 200 kwa kilo ktk bei elekezi ya 1000 pic.twitter.com/JMl4IV3Wl6
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#MWANANCHI Mahakama yabatilisha ndoa chini ya miaka 18, yaamuru umri wa kuolewa uwe kuanzia 18 na kuendelea pic.twitter.com/wdI4rdqI4l
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#JamboLEO TFDA imesema Mkoa wa Mbeya unaongoza kupitisha vipodozi feki vinavyosababisha saratani ya ngozi pic.twitter.com/HPGNyXDmMZ
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#HabariLEO Utafiti umebaini kuwa 51% ya walimu nchini ni watoro, baadhi hawaingii kabisa darasani pic.twitter.com/TUT1iPGp1r
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#HabariLEO Jeshi la polisi Dodoma linawashikilia viongozi watatu wa BAVICHA kwa uchochezi na kuikashifu Serikali pic.twitter.com/roypv4E0uT
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#MAJIRA Mtatiro asema hakubaliani na uamuzi wa Prof. Lipumba kutaka kuwania tena nafasi ya uenyekiti CUF pic.twitter.com/lzXTPx18jJ
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
#NIPASHE Waliohusika na kashfa zikiwamo 10 zilizolikumba taifa kuwa miongoni mwa watakaoanza mahakama ya mafisadi pic.twitter.com/kHSJAGuGRr
— millardayo (@millardayo) July 10, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 10 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI