Swali litakaloleta utata kwenye majibu ni kwamba kati ya wanawake na wanaume ni jinsia gani huwa wanaendesha magari yao vibaya na kusababisha ajali?
Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Michigan umeonyesha kwamba wanawake wanapata ajali nyingi zaidi ya wanaume japokuwa idadi ya madereva wa kike ni ndogo sana ukifananisha na wakiume.
Matokeo ya uchunguzi wao unasema kwamba wanawake wanatengeneza 40% ya madereva wote barabarani na wanaume wanachukua asilimia 60.
Wachunguzi hao wanasema kwamba maeneo ambayo wanawake wanapata sana ajali ni kwenye highway, crossroads na T-junctions.
Matokeo yote kwa ujumla yamewapa hitimisho la kwamba wanawake wanapata/husababisha ajali nyingi za barabarani licha ya kuwa wanawake wanaondesha magari idadi yao ni ndogo ukifananisha na ya wanaume.
Unasemaje kuhusu haya matokeo ya uchunguzi?…comment mawazo yako.