Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) mapema leo lilitangaza kuahirishwa kwa michuano ya mataifa Ulaya (Euro 2020) yaliyokuwa yafanyike kipindi cha majira ya joto mwaka huu.
UEFA wametangaza kuahirisha michuano hiyo hadi mwaka 2021 sasa itakuwa ni Euro 2021 sio 2020 tena, hata hivyo UEFA pia inapanga kumaliza michuano yote ya vilabu Ulaya June 30 endapo maambukizi ya corona yatazidi.