Waandamanaji zaidi ya 20,000 wamekusanyika katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Paris kudai haki itendeke katika kifo cha Mfaransa mweusi Adama Traore (24) aliyefia mikononi mwa Polisi mwaka 2016.
Uchunguzi wa mazingira ya kifo cha Traore umekuwa ukiendelea kwa miaka takriban minne huku kukiwa na ripoti zinazopingana kuhusu kile kilichosababisha kifo chake. Kisa cha Traore kimekuwa ushahidi mkubwa kuonesha ukatili unaofanywa na Polisi nchini humo.