Wanakijiji wa Kijiji cha Lwanyange, Uganda wamelalamikia kitendo cha Polisi wa eneo hilo kuwanyanyasa ikiwemo kuwapiga ambapo kutokana na hali hiyo Kijiji hicho kitabaki bila watu kutokana watu kuhama kwa hofu ya kunyanyaswa na Askari wa Jeshi la nchi hiyo.
Wanakijiji hao wamesema manyanyaso ya Polisi yamefanya watu wengi kubaki na ulemavu huku uongozi wa kijiji hicho ukionekana kutochukua hatua yoyote kusaidia hilo.
Mongi Vicent ni mmoja ya watu ambao wamepata ulemavu kutokana na kupigwa na Polisi, amesema imekuwa bahati kwake kuwa hai kutokana na Polisi kumtishia kumuua.
Kamanda wa Polisi katika eneo hilo Moses Akena ameahidi kufanya uchunguzi ili kujua maafisa waliohusika kwenye vitendo hivyo na kuharibu sifa ya Jeshi la Polisi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook