Kwa upande wa wapenzi wa Michezo na Watanzania kwa ujumla kuna taarifa ya majonzi ambayo imeripotiwa muda mfupi uliopita inahusu msiba wa mmoja wa watu ambao waliwahi kuwa makocha kwenye timu mbalimbali Tanzania pamoja na timu ya Taifa.
Taarifa hiyo inahusu msiba wa Kocha Sylvester Marsh ambaye amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Marehemu Marsh aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Kilimanjaro Stars pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Taarifa za awali zinasema Marehemu alikuwa akiugua lakini haikuwa inafahamika na watu wengi huku mdau mmoja Abdulfatah Saleh ambaye ni mmiliki wa Hoteli Kariakoo Dar es Salaam akijitolea kumhudumia katika matibabu yake.
Chanzo cha Stori: http: Saleh Jembe Blog
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook