Umoja wa Uzalendo Kwanza ambao unaundwa na wasanii wa BongoMovie, wachezaji wa zamani na waimbaji wa Muziki katika harakati zao za kuendelea kuhamasisha uzalendo kwa watanzania na kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli, walifanikiwa kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Baada ya kufanikiwa kufika Handeni ikiwa ni siku moja imepita toka watoke Tanga Mjini kutoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 29, wamepata bahati kwa DC Gondwe ambaye ameamua kuwapa shamba la hekari 130 na kuwafahamu kuwa ardhi ya Handeni wataalam wamechunguza inakubali mzao mbalimbali.
“Katika nchi ya viwanja ambayo Mh Rais anaipigania sana Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegela ameleta wawekezaji wa mazao ya matunda, Handeni matunda yanakuwa vizuri sana kwa mfano ardhi ya Handeni mnayoiona hapa ina uwezo wa kuzalisha nanasi bora kuliko nanasi linalozalishwa Kusini mwa Marekani” >>>DC Gondwe
VIDEO: Wasanii wa Uzalendo Kwanza wametoa Tsh Milioni 29 Bure!!! kwa ajili ya Tanga