Show ya XXL inayorushwa na Clouds FM Soudy Brown a.k.a Gossip Cop katoboa kuhusu kile ambacho alikiandia Linex kwenye ukurasa wake wa Facebook msanii Linex kumdai hela kiasi cha shilingi milioni 11 ambazo alimpatia ili amuuzie gari.
Gossip Cop ameongea na Linex ambaye amesimulia namna ambavyo msanii Steve Nyerere alimkutanisha na Nyamihela kwa ajili ya kumuuzia gari, ambapo Linex amesema magari ambayo alipewa na jamaa huyo hayakuwa yanaendana na kiwango cha pesa alichokitoa hivyo akamtaka amtafutie gari nyingine ambapo hakumpatia gari wala kumrudishia pesa milioni kumi aliyompatia.
Nyamihela amesema kuwa alimpatia gari Linex huku akiwa hajamalizia malipo ya pesa ambayo walikubaliana na baadaye aliamua kuchukua gari lake na kumrudishia pesa shilingi milioni moja na kiasi kilichobakia anasema ni milioni mbili tu na sio milioni kumi kama ambavyo msanii huyo anadai.
Mahusiano yao mbali na biashara hiyo Nyamihela amesema aliwahi kumsaidia mara kadhaa Linex kwenye shughuli zake za muziki.
Nimekuwekea hapa sauti niliyoirekodi kwenye U Heard, unaweza kuisikiliza hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook