Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha DAR na kuleta maafa ya mafuriko kwa baadhi ya sehemu, nyumba ya kifahari ya msanii Diamond Platnumz ambayo ujenzi wake haujakamilika nayo imekumbwa na madhara ya mvua baada ya ukuta wake kuanguka.
Mtaalam wa majengo fundi Saidi amesema tukio kama hilo linaweza kutokea kutokana ukuta kutowekwa zege la kutosha chini, na juu inawezekana hapakufungwa mkanda.
Soudy Brown alimtafuta Diamond lakini hakuweza kumpata kwenye simu kwa muda mrefu, akamtafuta meneja wake ambaye ni Said Fella.
Fella amesema ni kweli ukuta wa nyumba hiyo umeanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha lakini bado iko chini ya mkandarasi na anatakiwa kukabidhi mwezi wa sita kwa hiyo kuhusu suala la ukarabati liko mikononi mwao.
Ili kusikiliza story yote bonyeza play hapa chini…
https://soundcloud.com/millard_ayotv/u-heard-march-24
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook