Vijana waliokuwa wanasoma katika Chuo cha Filamu cha TFTC Ubungo, kinachomilikiwa na muigizaji Pastor Myamba, wamemtafuta Soudy Brown na kumuelezea malalamiko yao kuwa toka wamalize masomo kwenye chuo hicho hawajakabidhiwa vyeti mpaka sasa.
Wanafunzia hao wamesema walisoma katika Chuo hicho kozi ya miezi sita mwaka 2013, lakini mpaka leo hawajakabidhiwa vyeti wala kucheza filamu kama walivyoahidiwa na waliopewa vyeti walipoenda kutafuta kazi waliambiwa kuwa ni feki.
Wanafunzi hao wamesema baada ya Pastor Myamba kupata tetesi za malalamiko yao, walishangaa anawaandikia ujumbe mzito akielezea kusikitishwa kwake na taarifa za baadhi ya wanafunzi kutaka kumkodishia majambazi ili wamuue yeye na familia yake, ujumbe ambao wanafunzi hao wamesema ni kama vitisho kwao, Soudy alimtafuta Pastor Myamba lakini simu yake haikupatikana.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story yote…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook